Ofisa wa UM asistiza hitaji la nyenzo za kimataifa kuzuia uhamishaji usio halali wa silaha duniani
2023-04-11 18:30:57| cri

Ofisa mwandamizi wa ofisi ya upokonyaji silaha ya Umoja wa Mataifa Bi. Izumi Nakamitsu, amesisitiza kuwa utekelezaji wa makubaliano mbalimbali ya kimataifa kuhusu kudhibiti biashara na uhamishaji usio halali wa silaha ni muhimu katika kuhakikisha silaha haziendi kwa makundi yanayozitumia vibaya.

Amezitaka nchi wanachama kutekeleza kikamilifu majukumu yao chini ya makubaliano walioyasaini, na kujenga mifumo thabiti ya kudhibiti usafirishaji, udalali, uhifadhi na uhamishaji usio halali wa silaha na risasi. Amesisitiza kuwa uwazi wa usafirishaji wa silaha unaweza kutumika kama hatua ya kujenga imani kati ya nchi na kupunguza mivutano, utata, na kuelewana vibaya."