Mkurugenzi wa idara ya huduma za wakimbizi katika Wizara ya Mambo ya Ndani ya Tanzania, Sudi Mwakibasi amesema, raia 7,645 wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) wamekimbilia nchini Tanzania kutoka mashariki mwa nchi hiyo.
Akitoa taarifa kwa Waziri wa Mambo ya Ndani wa Tanzania Hamad Masauni alyekuwa akitembelea kambi za wakimbizi, Bw. Mwakibasi amesema wengi wa raia wa DRC wanaokimbilia nchini Tanzania wanatokea mkoa wa Kivu, mashariki mwa DRC, ambako vurugu zimeongezeka, na kwamba wakimbizi 5,465 kutoka DRC wamepata hifadhi katika kambi za wakimbizi mkoani Kigoma, magharibi mwa Tanzania.
Amesema idadi ya Wakongo wanaokimbilia nchini Tanzania imeongezeka kutoka 2,643 mwezi Machi na kufikia 7,645 April 7.