Kundi la upatanishi latoa mapendekezo mapya la kumaliza vita nchini Mali
2023-04-11 08:38:12| CRI

Msemaji wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Stephane Dujarric amesema, pande zilizosaini Makubaliano ya Amani ya Algiers ya mwaka 2014 zimetoa mapendekezo mapya ya kujadiliwa, siku moja kabla ya kikao cha Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kuhusu Mali kufanyika.

Dujarric amesema, kundi la kimataifa la upatanishi limewasilisha mapendekezo hayo kwa pande husika ili kuanza tena utekelezaji wa makubaliano ya amani. Amesema kundi hilo linalojumuisha Tume ya Umoja wa Mataifa nchini Mali, Algeria, Umoja wa Afrika, Jumuiya ya Uchumi ya Nchi za Afrika Magharibi, Umoja wa Ulaya, Marekani na Ufaransa, limeeleza wasiwasi wake kuhusu mvutano kati ya pande zilizosaini makubaliano hayo, makundi ya waasi na serikali.

Ameongeza kuwa, kundi hilo pia limerejea tena ahadi yake ya kuendelea kufanya kazi na makundi yaliyosaini makubaliano hayo na watu wa Mali katika nia yao ya kutafuta amai, utulivu na maridhiano ya kudumu.