Serikali ya Yemen yakaribisha Saudi Arabia kufanya mazungumzo ya amani na kundi la Houthi
2023-04-11 21:30:11| cri

Serikali ya Yemen imesema inakaribisha ujumbe wa Saudi Arabia kufanya mazungumzo ya amani na kundi la Houthi, na kutarajia matokeo mazuri. Pia imesema baada ya Saudi Arabia na Iran kurejesha uhusiano wa kidiplomasia, uwezekano wa amani nchini Yemen umekuwa mkubwa zaidi kuliko wakati wowote hapo awali.

Tarehe 9 mwezi huu, ofisa mwandamizi wa kundi la Houthi Mahdi al-Mashat alikutana na ujumbe wa Saudi Arabia uliongozwa na balozi wa nchi hiyo nchini Yemen Mohammed bin Saeed Al-Jaber huko Sana’a wakizungumzia masuala mbalimbali ikiwemo kusaini upya makubaliano ya kusitisha mapigano yaliyomalizika mwezi Oktoba mwaka jana.