Ethiopia yaweka vizuizi katika mji mkubwa wa kaskazini kutokana na vurugu
2023-04-11 08:37:34| CRI

Mamlaka katika mkoa wa Amhara, kaskazini mwa Ethiopia zimeweka vizuizi katika mji wa Gonder mkoani humo, ambapo bajaji zimezuiwa kufanya kazi nje ya kipindi cha kuanzia saa kumi na mbili asubuhi hadi saa mbili usiku, huku baa na vilabu vya usiku zikitakiwa kufungwa saa tatu usiku.

Vizuizi hivyo vimewekwa wakati maandamano yalipoanza wiki iliyopita yakiendelea katika miji mbalimbali ya mkoa wa Amhara dhidi ya mpango wa serikali kuu wa kuvunja vikosi maalum vya usalama katika mkoa huo.

Katika taarifa yake, Waziri Mkuu wa Ethiopia Abiy Ahmed amesema, serikali ya nchi hiyo inapanga kuhusisha vikosi maalum katika mikoa 11 ya nchi hiyo na idara nyingine za usalama kwa lengo la kuunda mfumo wa usalama wenye nguvu na umoja.