Naibu waziri wa habari, mawasiliano na teknolojia ya habari wa Tanzania Bw. Mathew Kundo amesema Tanzania inapanga kuweka WIFI kwenye maeneo ya umma ili kuhimiza matumizi ya teknolojia ya mawasiliano ya habari.
Akizungumza jana katika mkutano wa Bunge unaoendelea nchini humo, Bw. Kundo amesema serikali ya Tanzania inawekeza katika habari za kidigitali ili kuunga mkono maendeleo ya uchumi.
Pia amesema, serikali imetambua kuwa ni lazima kutoa huduma ya wazi ya WIFI, ili raia waweze kushiriki kwenye masuala ya jamii na uchumi, hatua itakayosaidia kuhimiza maendeleo na biashara.