Rais wa Ufaransa: Ulaya yatakiwa kuwa na uwezo wa kujiamulia wa kuchagua wenzi wa ushirikiano
2023-04-12 18:00:42| cri

Rais Emmanuel Macron wa Ufaransa ambaye yuko ziarani nchini Uholanzi ametoa hotuba akisisitiza kuwa Ulaya inatakiwa kudumisha ufunguaji mlango, huku ikilinda mamlaka ya uchumi. Kwa njia hiyo tu, ndio inaweza kujichagulia wenzi wa ushirikiano na kushika hatma yake mikononi mwa watu wa Ulaya.

Amesema, uhuru na kujiamulia ni muhimu kwa Ulaya, bara hilo linatakiwa kudumisha mtindo wake wa kujiendeleza na kutotegemea nchi nyingine.

Anaona kuwa kama Ulaya ikitaka kujihakikishia ushindani, inatakiwa kuimarisha uvumbuzi na mageuzi na kuongeza uwekezaji katika sekta ya elimu, ikiwemo kuongeza mafunzo ya kiufundi kwa nguvukazi za nchi mbalimbali barani Ulaya, na kuunganisha soko la Ulaya ili kuvutia mitaji na watu wenye ujuzi. Amesema Ulaya inatakiwa kuendeleza teknolojia ya juu na kuonya kuwa kutegemea teknolojia za nchi nyingi kutaifanya ikabiliwe na hatari.