Mazungumzo ya amani nchini Yemen yaendelea huku pande husika zikionyesha mtazamo chanya
2023-04-12 19:01:35| cri

Kundi la Houthi na ujumbe wa Saudi Arabia sasa wanafanya mazungumzo rasmi ya moja kwa moja huko mji wa Sana’a nchini Yemen ambapo pande husika zimeonyesha mtazamo chanya.

Balozi wa Saudi Arabia nchini Yemen Mohammed bin Saeed Al-Jaber anayeongoza ujumbe huo amesema kuwa Saudi Arabia inafanya juhudi za kutafuta njia za mazungumzo kati ya pande mbalimbali husika za Yemen na kuhimiza ufumbuzi kamili wa kisiasa na wa kudumu upatikane. Kiongozi wa kundi la Houthi Mohammed Ali al-Houthi pia ametoa taarifa kupitia televisheni akieleza kufanya mazungumzo na upande wa Saudi Arabia.

Msemaji wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Bw. Dujarric alisema kwamba mazungumzo hayo ni "hatua inayokaribishwa ya juhudi za kupunguza mvutano."