IMF yakadiria kuwa uchumi wa China utakua kwa asilimia 5.2 mwaka huu
2023-04-12 08:40:59| CRI

Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF) limetoa ripoti mpya kuhusu makadirio ya uchumi wa dunia, likikadiria kuwa uchumi wa China utakua kwa asilimia 5.2, na kuchangia maendeleo ya uchumi wa dunia.

Mshauri wa uchumi ambaye pia ni mkurugenzi wa Idara ya Utafiti ya IMF Pierre-Olivier Gourinchas amesema, hatua ya China kulegeza sera za kukabiliana na mlipuko wa COVID-19 imesaidia uchumi wa China kufufuka kwa kasi, na China itakuwa injini muhimu ya ukuaji wa uchumi wa dunia. 

Kwa mujibu wa ripoti hiyo, uchumi wa dunia unakadiriwa kukua kwa asilimia 2.8 mwaka 2023, ikiwa imeshuka kwa asilimia 0.1 ikilinganishwa na makadirio ya awali. Uchumi wa masoko yanayochipuka na nchi zinazoendelea unakadiriwa kukua kwa asilimia 3.9 mwaka huu, na uchumi wa nchi zilizoendelea utakua kwa asilimia 1.3 mwaka huu na asilimia 1.4 mwaka 2024.