Watu 134 wauawa na watu wenye silaha kusini mashariki mwa Nigeria
2023-04-12 08:38:33| cri

Gavana wa Jimbo la Benue, kusini mashariki mwa Nigeria, Bw. Samuel Ortom amesema, watu 134 wameuawa katika mashambulizi yaliyofanywa na watu wenye silaha katika vijiji vya jimbo hilo katika siku za hivi karibuni.

Rais wa Nigeria Muhammadu Buhari amelaani mauaji yaliyofanywa na watu hao dhidi ya raia wasio na hatia katika Jimbo la Benue, na kutaka washambuliaji hao wafikishwe mahakamani haraka iwezekanavyo.