Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amefanya ziara nchini Somalia ili kuunga mkono juhudi za kutafuta amani, usalama na misaada ya kibinadamu.
Katika ziara hiyo, Guterres amekutana na rais wa Somalia Hassan Sheikh Mohamud na kujadiliana kuhusu juhudi za serikali ya Somalia katika kukabiliana na ugaidi na kuhakikisha amani na usalama kwa kila mwananchi, na kwamba wamesisitiza umuhimu wa uratibu wa nguvu kati ya serikali kuu na majimbo ya nchi hiyo.
Kwa upande wake, rais Mohamud amesema, watu wa Somalia wanaushukuru Umoja wa Mataifa kwa kuwa mwenza wa Somalia kwa miongo kadhaa. Pia amesisitiza juhudi za kuikomboa nchi hiyo na vitendo vya kigaidi, kukwepa baa la njaa na migogoro ya kibinadamu, na pia kumaliza mageuzi ya kifedha na kiuchumi, mambo ambayo yamepewa kipaumbele na serikali yake.