Tanzania kujenga kiwanda cha kwanza cha kusafisha maji taka
2023-04-12 22:58:11| cri

Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira jijini Dar es Salaam (DAWASA) imeipa kampuni ya Metito, inayoongoza kwa kutoa huduma bora za maji, mkataba wa kusanifu, kujenga na kuendesha mtambo mpya wa kusafisha maji taka (WWTP) jijini Dar es Salaam.

Mradi huo utakaoanzishwa kwenye eneo la Mbezi Beach, unafadhiliwa na serikali kwa kushirikiana na Benki ya Dunia. Unatarajiwa kupunguza uchafuzi wa mazingira kupitia usafishaji salama wa maji taka.

Mtambo wa kusafisha maji taka utakuwa chini ya uhandisi na teknolojia ya hali ya juu ili kuongeza gharama za uendeshaji na matengenezo, kuongeza ubora wa tope na kupunguza kiwango cha jumla cha kaboni.

Kwa mujibu wa Kaimu Ofisa Mtendaji Mkuu wa DAWASA, Kiula Kingu, mtambo huo utasanifiwa ili kutosha karibu nusu ya eneo lililotengwa, kuwezesha matumizi bora ya ardhi na kuongeza akiba.

Alisema kampuni ya Metito yenye makao yake Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE) itafanya kazi ya uendeshaji wa miaka mitatu na matengenezo ya mtambo wa kusafisha maji taka kwa ushiriki kamili wa wafanyakazi wa DAWASA katika vitengo vyote vya kiwanda hicho.