Jaji wa Kenya na mtaalamu wa kiufundi kutoka Burundi ndio washindi wa kwanza wa Tuzo ya Uwajibikaji kwa Vitendo ya Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) 2022.
Shirika la Independent Recourse Mechanism (IRM) la AfDB lilitangaza washindi wa tuzo hizo, likiwataja Prof. Nixon Sifuna wa Kenya na Mkurugenzi wa Wakala wa Barabara wa Burundi Prof. Regis Mpawenayo.
Ikizinduliwa mwaka 2022, tuzo hiyo ya kila mwaka inatambua watu binafsi na mashirika ambayo yametoa mchango mkubwa katika uwajibikaji wakati wa ushiriki wao kwenye mchakato wa kushughulikia malalamiko wa IRM.
Jaji Sifuna ni jaji wa mazingira katika Mahakama Kuu nchini Kenya na wakili wa ngazi ya chini ambaye alitekeleza jukumu muhimu katika Mradi wa Majitaka wa AfDB wa Kapenguria-Makutano Towns, akiwakilisha zaidi ya watu 500 walioathiriwa na mradi huo katika malalamiko yaliyosimamiwa na IRM kupitia mchakato wake wa ukaguzi.
Kwa upande wake, Prof. Mpawenayo alibeba jukumu kubwa katika kutatua malalamiko yanayohusiana na Uboreshaji wa Barabara ya Nyakararo-Mwaro-Gitega (RN18) inayofadhiliwa na AfDB na Mradi wa Asphalting wa Awamu ya Pili wa Sehemu ya barabara ya Kibumbu-Gitega (Mweya) yenye urefu wa kilomita 24 nchini Burundi.