Bahrain na Qatar zaamua kurejesha rasmi uhusiano wa kidiplomasia
2023-04-13 08:26:13| cri

Bahrain na Qatar zimerejesha rasmi uhusiano wa kidiplomasia kati yao, ikiwa ni kuendana na kanuni za usawa wa pande zote na kuheshimu mamlaka na uhuru wa kila nchi, na kudumisha umoja ndani ya Baraza la Ushirikiano la Ghuba (GCC).

Wajumbe kutoka nchi hizo mbili wamekutana Riyadh, mji mkuu wa Saudi Arabia, ambapo pia waliamua kustawisha uhusiano kati ya nchi hizo kwa mujibu wa kanuni za Mkataba wa Umoja wa Mataifa na masharti ya Mkataba wa Vienna wa Mahusiano ya Kidiplomasia.