UNCTAD: kuongezeka kwa riba kupunguza zaidi ya dola bilioni 800 ya mapato ya nchi zinazoendelea
2023-04-13 22:30:11| cri

Ripoti iliyotolewa jana na Shirika la Umoja wa Mataifa la Biashara na Maendeleo (UNCTAD) imekadiria kwamba viwango vya juu vya riba duniani vitapunguza zaidi ya dola bilioni 800 katika mapato ya nchi zinazoendelea katika miaka ijayo.

Imeonya kuwa nchi zinazoendelea zinakumbwa na taabu wakati msukosuko wa fedha ukiongezeka na kasi ya ukuaji wa uchumi duniani ikipungua. Jumla ya ongezeko la GDP duniani la mwaka 2023 linakadiriwa kuwa asilimia 2.1 tu ambapo ukuaji wa uchumi katika sehemu kubwa ya dunia utapungua ikilinganishwa na wakati kabla ya janga la COVID-19.

Shirika hilo limetoa wito kwa jumuiya ya kimataifa kuweka ajenda ya kusaidia nchi zinazoendelea zikiwemo kufanya mageuzi ya muundo wa madeni duniani, kuongeza ukwasi na kutunga sheria na kanuni za kifedha zilizo kamili zaidi.