Tanzania na Kenya zakubaliana kupambana pamoja na bidhaa ghushi
2023-04-13 20:33:20| cri

Tanzania na Kenya zimekubaliana kushirikiana katika kupambana na bidhaa ghushi zinazoingia katika nchi hizo mbili ikiwa ni sehemu ya jitihada za kuwalinda wafanyabiashara na wawekezaji wanaojihusisha na bidhaa halisi.

Kwa mujibu wa Mkurugenzi wa Tume ya Ushindani Tanzania (FCC) William Urio, tume hiyo ilikamata bidhaa ghushi zenye thamani ya Sh15 bilioni katika mwaka wa fedha uliopita.

Nayo Mamlaka ya Kupambana na Bidhaa Ghushi ya Kenya (ACA) imesema, thamani ya biashara hiyo haramu nchini Kenya ilifikia Ksh800 bilioni (sawa na Tsh12.8 trilioni) mwaka 2020, huku bidhaa ghushi zikiwa na thamani ya Ksh100 bilioni.

Ni kwa misingi hiyo ambapo mataifa hayo mawili yalikutana juzi na kuona umuhimu wa kufanya juhudi za pamoja kukabiliana na changamoto hiyo ambayo ni tishio kwa wawekezaji na afya za watumiaji.