Kenya yaandaa jukwaa la matangazo la Maonyesho ya Canton kuwalenga wajasiriamali
2023-04-13 08:25:53| CRI

Matangazo ya kuvutia wajasiriamali wa Kenya kushiriki katika Maonyesho ya 133 ya Uagizaji na Uuzaji nje wa bidhaa ya China, yamefanyika jijini Nairobi jana jumatano, na kuvutia idadi kubwa ya washiriki wakiwemo wabunge na wajasiriamali wanaoibuka.

Meneja mkuu wa Idara ya uwekezaji na maendeleo ya biashara katika Mamlaka ya Uwekezaji ya Kenya Pius Rotich amesema, serikali ya Kenya inapenda kutumia fursa ya Maonyesho hayo kuimarisha biashara na kuvutia uwekezaji kutoka China kuendana na ajenda mpya ya mageuzi ya kiuchumi.

Amesema Maonyesho ya Canton yanatoa fursa kwa wajasiriamali wa Kenya kutafuta ushirikiano na wenzao wa China, kupata mitaji, teknolojia na ufahamu ili kuendeleza ukuaji wa sekta muhimu kama kilimo na viwanda.