Makubaliano ya RCEP kuanza kutumika kwa nchi wanachama wake wote mwezi Juni
2023-04-13 19:29:09| cri

Makubaliano ya Uhusiano wa Wenzi wa Kiuchumi wa Kikanda Kwa Pande Zote RCEP yataanza kutekelezwa nchini Ufilipino kuanzia tarehe pili mwezi Juni, ikimaanisha kuwa makubaliano hayo yatatekelezwa katika nchi wanachama wake wote 15 na hivyo eneo kubwa zaidi la biashara huria duniani litaingia katika kipindi kipya cha utekelezaji kamilifu.

Sasa biashara kati ya China na nchi wanachama wa RCEP imechukua asilimia 30.8 ya jumla ya biashara ya nje ya China. Kutekelezwa kwa makubaliano hayo kutasaidia kuimarisha mnyororo wa ugavi na viwanda wa kikanda na kuhimiza ustawi wa muda mrefu wa uchumi wa dunia.