China yatoa wito wa kuiunga mkono serikali ya Mali kuanzisha operesheni ya kupambana na ugaidi
2023-04-13 08:28:41| CRI

Mjumbe wa kudumu wa China kwenye Umoja wa Mataifa Balozi Zhang Jun amesema, jumuiya ya kimataifa inapaswa kuunga mkono serikali ya Mali kuanzisha operesheni ya kupambana na ugaidi, na kuhimiza utekelezaji wa makubaliano ya amani kuna umuhimu mkubwa kwa kulinda amani na utulivu nchini Mali.

Balozi Zhang amesema hayo katika Mkutano wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kuhusu suala la Mali, akisisitiza kuwa jumuiya ya kimataifa inapaswa kutoa kipaumbele katika kuiunga mkono Mali kupambana na ugaidi, kulinda utulivu na usalama wa raia, na kutoa misaada mingi zaidi katika mambo ya fedha, vifaa, habari na utoaji wa huduma.

Pia amesema China inapinga kutumia suala la haki za kibinadamu kuwa chombo cha kisiasa cha kuharibu operesheni za kigaidi, na haitakubali kuhusisha suala la haki za kibinadamu na uungaji mkono wa mapambano dhidi ya ugaidi, na kwamba vitendo kama hivyo si kama tu vinaharibu mamlaka ya Mali, bali pia havisaidii kulinda haki za kibinadamu.