Rais wa China akagua kikosi cha jeshi la majini Kamandi ya Kusini
2023-04-13 08:26:41| CRI

Rais wa China Xi Jinping jumanne wiki hii amefanya ukaguzi kikosi cha jeshi la majini la Jeshi la Ukombozi wa Watu wa China (PLA) Kamandi ya Kusini.

Akizungumza katika Makao Makuu ya Kamandi hiyo, Rais Xi ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati Kuu ya Kijeshi ya China, amesisitiza kuimarisha mafunzo na utayari wa mapambano, na pia kuongeza kasi ya mageuzi ili kuboresha ngazi ya kisasa kwa pande zote ya vikosi vya ulinzi. Ametoa wito kwa vikosi vya ulinzi kutimiza kikamilifu majukumu waliyopewa na Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) na wananchi.

Pia rais Xi amewataka askari hao kulinda mamlaka na ardhi ya China na haki na maslahi ya baharini, na kudumisha utulivu kamili wa maeneo ya jirani na China.