China kuendelea kutoa mchango kusaidia nchi za Kiarabu kufikia umoja
2023-04-14 08:46:30| cri

Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya China Bw. Wang Wenbin amesema, China inapenda kuendelea kutoa mchango mkubwa katika kuzisaidia nchi za Kiarabu kufikia umoja.

Bw. Wang amesema, China inakaribisha na kuthamini juhudi za Saudi Arabia, Oman na nchi nyingine za eneo hilo katika kutuliza hali ya Yemen na kufikia usitishaji vita wa kudumu, na kuunga mkono pande zinazohusika kufikia suluhu la kisiasa la suala la Yemen kwa njia ya mazungumzo.

Hivi karibuni, Saudi Arabia na Oman zilituma ujumbe kwa pamoja katika mji mkuu wa Yemen, Sana'a, kufanya mazungumzo na kundi la Houthi, kwa lengo la kumaliza mzozo wa Yemen uliodumu kwa miaka mingi.