Rais Xi Jinping wa China afanya mazungumzo na rais wa Brazil
2023-04-14 21:38:22| cri

Rais Xi Jinping wa China amefanya mazungumzo na rais Lula da Silva wa Brazil tarehe 14 mchana.

Rais Xi Jinping amesema, mwaka huu ni mwaka wa kwanza kwa China kutekeleza moyo wa Mkutano Mkuu wa 20 wa CPC. China itasukuma mbele maendeleo ya hali ya juu, kujenga utaratibu mpya wa maendeleo, kuhimiza ufunguaji mlango wa kiwango cha juu, na China italeta fursa nyingi zaidi kwa nchi mbalimbali duniani ikiwemo Brazil. Anaamini kuwa uhusiano kati ya China na Brazil unaopata maendeleo mazuri hakika utatoa mchango muhimu kwa amani, utulivu, ustawi na maendeleo ya kikanda na kimataifa.