Mamlaka ya Mchinji ya Malawi imethibitisha kuwa, takriban watu 17 wanahofiwa kufariki kwenye eneo hilo lililoko magharibi mwa Malawi, baada ya boti waliyopanda kuvuka mto kuzama Jumatano jioni.
Inasemekana kuwa boti hiyo ilikuwa na abiria 22 wakiwemo watu wazima 19 na watoto watatu ambao walikuwa wakivuka mto ili kuhudhuria mazishi. Shuhuda mmoja amesema boti hiyo iliyokuwa na uwezo wa kubeba watu 10, ilibeba watu 22, jambo linaloweza kuwa chanzo cha ajali hiyo.
Kwa mujibu wa Fred Movete, mkuu wa eneo hilo, na John Nkhoma, ofisa wa Kituo cha Polisi, watu watano walifanikiwa kufika kando ya mto kwa msaada wa wenyeji.
Juhudi za utafutaji na uokoaji zilizofanywa na wenyeji zilishindwa na wataalamu wa uokoaji wa baharini wanafanya zoezi la utafutaji na uokoaji.