Mkurugenzi wa Benki ya Dunia asema uchumi wa China unachangia ongezeko la uchumi wa dunia
2023-04-14 08:36:24| cri


 

Mkurugenzi wa Benki ya Dunia Bw. David Malpass jana amesema, licha ya ukuaji dhaifu wa uchumi wa dunia, uchumi wa China umeonyesha mwelekeo mzuri na unaotoa mchango mkubwa katika ukuaji wa uchumi wa dunia.

Bw. Malpass amesema hayo kwenye mkutano na waandishi wa habari kando ya Mkutano wa Majira ya Mchipuko wa Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF) na Benki ya Dunia.

Bw. Malpass amesema, ongezeko la uchumi wa China katika mwaka 2023 linakadiriwa kuongezeka kwa asilimia 5.1 kutoka asilimia 3 kwa mwaka 2022.