China yataka mapigano nchini Sudan yasimamishwe mapema
2023-04-16 17:27:12| CRI

Wizara ya Mambo ya Nje ya China imezitaka pande zinazopingana nchini Sudan kusimamisha mapigano mapema, ili kuzuia hali kuwa mbaya.

Katika taarifa yake, Wizara hiyo imezungumza mapigano kati ya kikosi cha Rapid Support Forces (RSF) na jeshi la serikali ya Sudan yaliyotokea jumamosi katika maeneo mengi ya mji mkuu wa nchi hiyo, Khartoum.

Pia Wizara hiyo imesisitiza kuwa, China inazitaka pande mbalimbali nchini Sudan ziimarishe mazungumzo ili kuhimiza kwa pamoja mchakato wa mpito cha kisiasa.