Tume ya Umoja wa Afrika nchini Somalia (ATMIS) imesema Jumapili kuwa imeanza kutoa mafunzo ya siku tano ili kuwapa ujuzi na elimu wafanyakazi wake wa kukabiliana na mahitaji yao ya afya ya akili na saikolojia wakati wanahudumu kwenye tume hiyo.
Mafunzo ya afya ya akili na saikolojia kwenye operesheni za amani yamewaleta pamoja maafisa wa polisi na jeshi ambao wapo kwenye maeneo ya vurugu, vifo na maangamizi, ambapo watajifunza kuhusu namna migogoro inavyoathiri afya ya akili, familia, jamii na matokeo ya kiwewe na sonona wanayopata baada ya walinda amani wa tume hiyo kupata taharuki, na namna ya kusimamia sonona wakati wanatumikia tume hiyo.
Mwakilishi maalumu wa Mwenyekiti wa Kamisheni ya Umoja wa Afrika nchini Somalia na mkuu wa ATMIS Mohammed El-Amine Souef wakati akifungua mafunzo hayo ametaja hatari na changamoto za afya ya akili wanazokabiliana nazo walinda amani.