Watu 40 wauawa katika shambulizi Burkina Faso
2023-04-17 09:22:29| CRI

Takriban watu 40 wameuawa na wengine 33 kujeruhiwa siku ya Jumamosi katika shambulizi dhidi ya kikosi cha kijeshi kaskazini mwa Burkina Faso.

Kwa mujibu wa taarifa ya katibu mkuu wa mkoa wa Kaskazini, kikosi hicho kilichoko karibu na kijiji cha Aorema, ambacho hakiko mbali na mji wa Ouahigouya, kilishambuliwa na watu wasiojulikana Jumamosi.

Hadi sasa idadi ya watu waliouawa imefikia 40, wakiwemo askari sita na wanajeshi 34 wa kujitolea.