Wachina husema, mpango wa kila mwaka unaanza katika majira ya mchipuko. Hivi sasa tupo kwenye majira ya mchipuko hapa Beijing, watu wanahangaika kupanda milima, kutembelea bustani za maua au kwenda picnic. Katika vipindi vitatu vijavyo, sisi tutarudia jinsi rais Xi Jinping wa China alivyotumia “majira ya mchipuko” kueleza sera zake.
"Ua moja linapochanua sio majira ya mchipuko, lakini maua mbalimbali yakichanua pamoja hufanya bustani kujaa katika majira ya mchipuko." Hii ni sehemu ya hotuba ya rais Xi Jinping kwenye mazungumzo ya ngazi ya juu ya CPC na vyama vingine vya kisiasa duniani yaliyofanyika tarehe 13, Machi mwaka 2023.