Namibia na China kujenga kwa pamoja kituo cha umeme wa upepo
2023-04-18 21:52:44| cri

Kampuni ya Uwekezaji ya Riminii ya nchini Namibia na kampuni ya Nishati ya China zimesaini makubaliano ya manunuzi na ugavi wa nishati ili kujenga kituo cha umeme wa upepo kitakachozalisha megawati 50 za nishati hiyo katika mji wa Luderitz, kusini magharibi mwa Namibia.

Shirika la Umeme la Namibia limesma katika taarifa yake kuwa, ujenzi wa kituo hicho utagharimu dola za kimarekani milioni 96.4, na unatarajiwa kukamilika ndani ya miezi 27, huku uzalishaji rasmi ukitarajiwa kuanza mwezi Julai, 2025.

Akizungumza katika hafla hiyo, Mkurugenzi Mkuu wa Shirika hilo Kahenge Haulofu amesema, mradi huo utatoa mchango mkubwa katika upatikanaji wa nishati, utakapounganishwa na miradi mingine ya umeme inayounda sehemu ya Mkakati wa Kina wa Mipango ya Biashara.