Wahudumu wa afya katika kaunti 12 za Kisumu, Mombasa, Taita Taveta, Vihiga, Embu, Nyandarua, Bomet, Laikipia, Nyeri, Murang’a, Kisii na Nyamira nchini Kenya wametangaza kuwa wataanza mgomo kesho jumatano hadi watakapolipwa mishahara yao ya mwezi wa Machi.
Wahudumu hao wakiwemo wauguzi, madaktari, maafisa wa kliniki, wamesema wamechoka kucheleweshewa mishahara yao kila mwezi.
Mgomo huo unatangazwa wakati Waziri wa Afya nchini Kenya, Bi Susan Nakhumincha, akisema serikali itatatua mzozo huo wa migomo ya kila mara, na kuongeza kuwa, serikali italitaka baraza la wafanyakazi wa Afya kutatua changamoto za wahudumu wa afya.