UM waeleza wasiwasi juu ya Marekani kumsikiliza kisiri Katibu Mkuu wake
2023-04-19 10:08:34| CRI

Msemaji wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Stephane Dujarric amesema kuwa Umoja huo umewasilisha rasmi wasiwasi wake kwa Marekani juu ya ripoti za kumfuatilia Katibu Mkuu Antonio Guterres.

Umoja wa Mataifa umeweka wazi kuwa vitendo kama hivyo haviendani na majukumu ya Marekani kwa mujibu wa Mkataba wa Umoja wa Mataifa na Mkataba wa Haki na Kinga wa Umoja huo.

Gazeti la Washington Post Jumatatu liliripoti kuwa kwa mujibu wa ripoti nne za siri lilizopata gazeti hilo, Marekani ilisikiliza na kukusanya taarifa za kijasusi kuhusu Guterres.

Kati ya nyaraka hizo, ambazo mbili hazijaripotiwa hapo awali, zinatoa muhtasari wa mazungumzo yaliyonaswa ambayo yanatoa habari mpya juu ya maingiliano ya Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa na maafisa wakuu wa UM na viongozi wa dunia.