Shirika la Idadi ya Watu la Umoja wa Mataifa (UNFPA) limesema, Ethiopia inaendelea kukabiliwa na changamoto kubwa za kibinadamu zinazotokana na majanga ya asili na ya kibinadamu.
Katika ripoti yake ya hivi karibuni kuhusu hali ya Ethiopia, UNFPA imesema nchi hiyo imeendelea kukabiliwa na changamoto kubwa za kibinadamu kutokana na mapigano na watu kukimbia makazi yao, ukame, mafuriko, na milipuko ya magonjwa. Ripoti hiyo imesema, ukosefu wa usalama wa chakula katika eneo la kaskazini mwa Ethiopia na majanga yanayoyakumba maeneo yaliyoathiriwa na ukame ni mambo yanayotishia na kuleta wasiwasi kwa afya ya watu katika maeneo hayo.
Kwa mujibu wa Mpango wa Msaada wa Kibinadamu wa mwaka 2023, zaidi ya watu milioni 20 wanakadiriwa kuhitaji msaada wa kuokoa maisha, huku watu milioni 10 wakikadiriwa kuhitaji huduma za ulinzi nchini Ethiopia.