Nigeria yaruhusu chanjo za Malaria za Oxford kutumika kwa watoto nchini humo
2023-04-19 18:57:45| cri

Nigeria itakuwa nchi ya pili barani Afrika kuridhia chanjo ya kuzuia malaria, ugonjwa unaoathiri na kusababisha vifo vya maelfu ya watu kwa mwaka nchini humo.

Tangazo hilo limetolewa jumatatu wiki hii na Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi na Udhibiti wa Madawa na Chakula nchini humo, Mojisola Adeyeye, ambaye amesema chanjo hiyo itasaidia kuzuia malaria kwa watoto wenye umri wa chini ya miaka mitano.

Chanjo hiyo ya malaria imebuniwa na Chuo Kikuu cha Oxford cha nchini Uingereza na kutengenezwa na Taasisi ya Chanjo ya Dawa ya nchini India, ilianza kutumika nchini Ghana.