Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi (UNHCR) na Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC), jumatatu zilisaini makubaliano (MoU) jijini Arusha, kaskazini mwa Tanzania, yenye lengo la kufufua na kuimarisha ushirikiano katika kushughulikia masuala ya wakimbizi na kukidhi mahitaji yao ya kupata makazi na ulinzi wa kimataifa.
Taarifa iliyotolewa na EAC imesema, ushirikiano huo unalenga kuziunga mkono nchi wanachama wa Jumuiya hiyo kuweka mazingira yatakayofaa kwa ufumbuzi wa kina wa watu kukimbia makazi yao, ikiwa ni pamoja na kuwarejesha makwao kwa hiari na kuwarejesha katika jamii.