Uongozi mkuu wa CPC waeleza mpango wa miaka mitano wa kuboresha kanuni za Chama
2023-04-19 10:05:52| CRI

Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) imeeleza muhtasari wa mpango wake wa kutoa na kurekebisha kanuni za Chama kuanzia mwaka 2023 hadi 2027.

Kwa mujibu wa muhtasari huo, uliotangazwa hadharani Jumanne, kipaumbele kimoja cha mpango huo ni kuboresha mifumo inayoshikilia nafasi ya msingi ya Xi Jinping kuhusu Kamati Kuu ya CPC na kwenye Chama kwa ujumla, na kushikilia mamlaka ya Kamati Kuu na uongozi wake unaozingatia umoja.

Taratibu za kuhakikisha uongozi wa Kamati Kuu juu ya mipango mikuu zitakamilika. Mifumo itawekwa ili kuhakikisha Kamati Kuu pekee ndiyo yenye haki ya kuamua na kueleza kanuni na sera kuu zinazohusu Chama na nchi nzima.

Aidha zitatolewa kanuni kadhaa kuhusu utekelezaji wa maamuzi na mipango mikuu ya Kamati Kuu, zikidhibiti kila kiungo kuanzia mgawanyo wa kazi hadi tathmini ya matokeo na usimamizi.