Watu 200 wauawa katika mapigano yanayoendelea nchini Sudan
2023-04-19 21:55:42| cri

Mapigano kati ya Wanajeshi wa Sudan (SAF) na Wanajeshi wa Msaada wa Haraka (RSF) nchini Sudan yamesababisha vifo vya takriban watu 200 na kujeruhi 1,800, kuharibu majengo ya Hospitali na kukwamisha misaada mjini Khartoum.

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Antonio Guterres amezitaka pande zinazopigana nchini Sudan kusitisha uhasama mara moja na kusema ongezeko la mzozo kati ya jeshi na makundi ya kijeshi, wakiongozwa na majenerali wapinzani, unaweza kuleta athari kubwa nchini humo na katika kanda hiyo.

Mapigano nchini Sudan yalizuka jumamosi kufuatia vita vya kugombania madaraka kati ya majenerali wawili waliohusika katika mapinduzi ya mwaka 2021, Mkuu wa jeshi la Sudan, Jenerali Abdel Fattah al-Burhan, na Makamu wake, Jenerali Mohamed Hamdan Daglo ambaye ni kamanda anayeongoza kikosi cha RSF.