MEI MOSI NA UHURU WA VYOMBO VYA HABARI
2023-04-28 08:01:00| CRI

Mei Mosi ya kila mwaka ni Siku ya Wafanyakazi Duniani, ambapo wafanyakazi hupata fursa ya kuwasilisha malalamiko na mapendekeo yao kwa viongozi husika ili vifanyiwe kazi. Pia, tarehe 3 Mei ni Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari, ambayo ilianza kuadhimishwa mwaka 1993. Hivyo basi, katika kipindi cha Ukumbi wa Wanawake siku hii ya leo, tunazungumzia suala la usawa wa jinsia katika sehemu za kazi, na pia ni nafasi ya mwanamke katika sekta ya habari.