Peng Liyuan akutana na mke wa rais wa Gabon
2023-04-20 09:00:37| CRI

Peng Liyuan, mke wa Rais Xi Jinping wa China, jana hapa Beijing alikutana na Sylvia Bongo Ondimba, mke wa Rais wa Jamhuri ya Gabon Ali Bongo Ondimba.

Akikumbuka mwingiliano wake na Sylvia na juhudi zao za pamoja za kukuza kinga na matibabu ya VVU/UKIMWI, Peng alisema anathamini hamasa ya muda mrefu ya Sylvia ya kutafuta ustawi wa umma.

Peng alieleza mafanikio ya China katika kuzuia na kutibu VVU/UKIMWI, kifua kikuu, na mapambano dhidi ya COVID-19, pamoja na kazi yake kama balozi mwema wa Shirika la Afya Duniani (WHO) wa kifua kikuu na VVU/UKIMWI.

Kwa upande wake, Sylvia, ambaye anafuatana na rais wa Gabon katika ziara yake ya serikali nchini China, aliwashukuru rais Xi na mkewe Peng kwa ukarimu wao na kusema kuwa anafurahishwa na uhusiano wa kirafiki wa China na Gabon. Alisema Gabon inasifu mafanikio makubwa ya China katika afya ya umma, na inapenda kujifunza kutokana na uzoefu wa China na kuimarisha mawasiliano na ushirikiano na China. Sylvia pia alisema anatarajia kupata fursa ya kuona mambo mengi zaidi ya China haswa utamaduni na maendeleo ya nchi hii.