China yasema misaada ya matibabu iliyotoa kwa nje ni misaada kati ya rafiki usio na masharti ya kisiasa
2023-04-20 21:29:23| cri

Msemaji wa Wizara ya mambo ya nje ya China Bw. Wang Wenbin amesema, misaada ya matibabu iliyotolewa na China kwa nje katika miaka 60 iliyopita, ni misaada ya kirafiki isio na masharti ya kisiasa na maslahi ya kikanda.

Bw. Wang amesema hayo jana alipokuwa akieleza mafanikio ya misaada ya matibabu inayotolewa na China kwa nchi za nje. Amesema, tangu China ilipotuma kikosi cha matibabu kwa Algeria mwezi Aprili mwaka 1963, China imetuma wahudumu wa afya elfu 30 wa vikosi vya matibabu kwa nchi na sehemu 76, na kutoa huduma za matibabu kwa watu milioni 290.