Watu wasiopungua 80 wafariki kwenye mkanyagano nchini Yemen
2023-04-20 09:05:20| CRI

Msemaji wa Wizara ya Afya inayoongozwa na Houthi Anis Al-Subaihi alisema mkanyagano ulitokea Jumatano usiku kwenye kituo cha utoaji wa msaada kilichoko Sanaa, mji mkuu wa Yemen, umesababisha vifo vya watu wasiopungua 80, na wengine 220 kujeruhiwa.

Kwa mujibu wa Wizara ya Mambo ya Ndani inayodhibitiwa na Houthi, mkanyagano huo ulisababishwa na wafanyabiashara waliogawa fedha kiholela bila uratibu wa Wizara hiyo.

Wayemen wengi ambao wamekuwa fukara kutoka na migogoro inayoendelea kwa miaka mingi, walimiminika kwenye vituo vya misaada ili kujipatia mahitaji ya kimsingi wakati sikukuu ya Eid al Fitri ikikaribia.