Umoja wa Mataifa wasema watu zaidi ya 150 wameuawa mkoani Ituri, DRC katika wiki mbili zilizopita
2023-04-20 21:27:23| cri

Umoja wa Mataifa umesema, watu zaidi ya 150 wameuawa katika mashambulizi kwenye mkoa wa Ituri, mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) katika wiki mbili zilizopita.

Ofisi ya Umoja wa Mataifa inayoratibu Masuala ya Kibinadamu (OCHA) imeonya juu ya kuendelea kwa mashambulizi dhidi ya raia katika wilaya za Djugu, Irumu na Mambasa, ambayo yamesababisha vifo vya raia zaidi ya 150 tangu mwanzo wa mwezi huu.