Watendaji wa benki: Uwekezaji wa China ni muhimu katika kuleta utulivu wa uchumi wa Kenya
2023-04-20 09:04:26| CRI

Watendaji wakuu wa Benki ya Absa wamesema mtiririko endelevu wa mtaji na biashara na China vitakuwa muhimu katika kuleta utulivu wa uchumi wa Kenya kufuatia kuwepo kwa mivutano ya siasa za kijiografia, mfumuko wa bei duniani, na deni kubwa la umma,

Antony Mulisa, mweka hazina wa kanda ya Afrika Mashariki katika Benki ya Absa, alisisitiza kwamba Kenya inapaswa kutumia uwekezaji wa China na kuimarisha biashara na nchi hii ili kuingiza uhai mpya katika uchumi na kueneza ustawi kwa wananchi wote.

Mulisa alibainisha kuwa kutokana na njia mseto zinazoendelea, uchumi wa Kenya unaweza kuvutia uwekezaji endelevu kutoka China, na kuulinda dhidi ya majanga mbalimbali kama vile ukame wa muda mrefu na kukatika kwa mnyororo wa usambazaji unaohusishwa na mgogoro wa Ukraine.