WHO yaipongeza Tanzania kwa kuongeza utoaji chanjo ya UVIKO-19
2023-04-21 10:03:35| CRI

Shirika la Afya Duniani (WHO) limeipongeza Tanzania kwa kuongeza utoaji chanjo ya UVIKO-19.

Taarifa iliyotolewa na Ofisi ya WHO Tanzania jijini Dar es Salaam, ilisema wakati utoaji wa chanjo ya UVIKO-19 ukiingia katika hatua ya kuunganishwa na huduma za kawaida, Tanzania imekuwa nchi inayofanya vizuri zaidi kati ya nchi 34 za Afrika zilizokuwa na idadi ya chini ya asilimia 10 ya watu wote waliolengwa hadi Januari 2022.

WHO, Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto UNICEF, na Muungano wa Chanjo (Gavi), walizindua Ushirikiano wa Kutoa Chanjo ya UVIKO-19 (CoVDP) Januari 2022 ili kuwezesha chanjo hiyo kutolewa kwa haraka na kulinda jamii zenye utendaji duni katika kuchanja watu wake.