Sudan Kusini yaunda timu ya dharura kuendelea na uzalishaji wa mafuta kufuatia mzozo wa Sudan
2023-04-21 10:04:51| CRI

Sudan Kusini imeunda timu ya kukabiliana na dharura kwa ushirikiano na makampuni yanayozalisha mafuta ili kuhakikisha uzalishaji endelevu wa mafuta kufuatia kuzuka kwa vita nchini Sudan mwishoni mwa juma lililopita.

Waziri wa Petroli, Puot Kang Chol, alisema timu hiyo inaongozwa na mpango wa dharura ulioandaliwa na kuanishwa vizuri ambao utapunguza kwa vitendo ukali wa athari za mapigano nchini Sudan kwa kupitisha njia tofauti vifaa na usafirishaji wa vitu vyote muhimu na kemikali wakati mzozo umeanza kuathiri taratibu za usambazaji na usafirishaji wa nyenzo na vifaa muhimu kupitia Bandari ya Sudan hadi maeneo ya mafuta huko Sudan Kusini.

Kang amesema vifaa vyote vya maeneo ya mafuta kama vile mabomba, pampu za kusukuma mafuta, mitambo ya uchakataji, vifaa vya juu ya ardhi na kituo cha usafirishaji nje cha baharini nchini Sudan, vimelindwa vizuri na salama ili visipate uharibifu wowote, na vinaendelea kuzalisha na kuuza nje wastani wa mapipa 169,140.81 ya mafuta ghafi kwa siku kutoka maeneo yote ya mafuta nchini Sudan Kusini.