Katibu mkuu wa UM atoa wito wa kusitisha vita kwa siku tatu nchini Sudan
2023-04-21 10:02:27| CRI

Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Bw. Antonio Guterres ametoa wito wa kusitisha vita kwa siku tatu za sikukuu ya Eid al Fitr nchini Sudan, ili kuruhusu raia waliokwama waondoke na kutafuta matibabu, chakula na bidhaa nyingine za kimsingi.

Aliongeza kuwa hiyo lazima iwe hatua ya kwanza katika kutandika njia ya kukomesha vita, na kusisitiza kuwa baada ya kusimamisha mapambano, ni lazima kufanya mazungumzo kwa makini, ili kutimiza mpito wenye mafanikio.