Katibu wa Idara ya Habari na Uenezi ya chama tawala nchini Zimbabwe (ZANU PF) Christopher Mutsvangwa amesema, Pendekezo la Ukanda Mmoja, Njia Moja la China linazisaidia nchi nyingi za Afrika kunufaika na maendeleo ya China.
Akizungumza katika mahojiano na Shirika la Habari la China (Xinhua), Mutsvangwa amesema, katika miaka 5,000 iliyopita, Afrika, Asia na Ulaya zimeendelea kukuza ustaarabu wa binadamu, na Pendekezo hilo limesaidia zaidi katika kupanua muunganiko kati ya mabara hayo.
Naye mtafiti katika Kituo cha Afrika cha Elimu ya Marekani katika Chuo Kikuu cha Witwatersrand nchini Afrika Kusini, Gideon Chitanga amesema, Pendekezo hilo limeimarisha msingi wa uhusiano kati ya nchi za Afrika na China, hususan katika ushirikiano wa ujenzi wa miundombinu.
Kwa mujibu wa Benki ya Maendeleo ya Afrika, pengo la uwekezaji wa miundombinu katika bara hilo linakadiriwa kuwa zaidi ya dola za kimarekani bilioni 100 kwa mwaka, na kuathiri mazingira ya maisha ya Waafrika na uwezo wa ushindani wa bara hilo duniani.