Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa atoa wito wa kuharakishwa kwa hatua za kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi
2023-04-24 08:42:28| cri

Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Bw. Antonio Guterres ametoa wito kwa jumuiya ya kimataifa kuharakisha hatua za kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi, na kuzitaka nchi mbalimbali kutoa mchango muhimu katika kulinda mazingira.

Guterres amesema hayo wakati wa maadhimisho ya Siku ya Dunia tarehe 22 mwezi huu. Amesema, jamii ya kimataifa inapaswa kuchukua hatua za kupunguza utoaji wa hewa chafu kwa undani zaidi na kwa haraka zaidi, na kupunguza ongezeko la joto duniani hadi nyuzi joto 1.5. Pia amesema, inapaswa kuongeza kwa kiasi kikubwa uwekezaji katika uwezo wa ustahimilivu, hasa katika nchi zilizo hatarini zaidi na jamii ambazo hazihusiki zaidi na uchafuzi wa hali ya hewa.