Jeshi la Sudan na jeshi la RSF zimelaumiana kwa kufanya mashambulizi dhidi ya misafara ya wanadiplomasia wa kigeni nchini humo.
Katika taarifa yake iliyotolewa jana jumapili, jeshi la Sudan lililishutumu jeshi la RSF kwa kufyatulia risasi misafara iliyokuwa ikiwaondoa wafanyakazi wa balozi za Qatar na Ufaransa.
Hata hivyo, jeshi la RSF lilijibu tuhuma hizo, likisema msafara wa raia wa Ufaransa ulishambuliwa kutoka angani na vikosi vya waasi wakati raia hao wakiondolewa nchini humo. Pia jeshi hilo limesema linashikilia ahadi yake ya kusimamisha vita, kufungua njia za kuwawezesha watu kupata mahitaji muhimu na huduma za afya, na kuhakikisha raia wa kigeni wanaondolewa salama kutoka nchini humo.