China yaazimia kutekeleza masuala waliyokubaliana na Tanzania
2023-04-24 18:20:30| cri

China imeonesha utayari wa kushirikiana na Tanzania katika kutekeleza masuala yote yaliyofikiwa kati ya Rais Xi Jinping na mwenzake Samia Suluhu Hassan, yakiwa ni pamoja na kuzidisha mawasiliano na ushirikiano kati ya vyama, na kukuza maendeleo zaidi ya uhusiano kati ya China na Tanzania na China na Afrika.

Hayo yamebainishwa na Mkurugenzi wa Ofisi ya Tume ya Mambo ya Nje ya Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) Wang Yi alipokutana na washiriki wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) kwenye mkutano ulioongozwa na Katibu Mkuu wa CCM Daniel Godfrey Chongolo.

Mkutano huo uliofanyika siku ya Ijumaa katika Ukumbi Mkuu wa Mikutano ya Umma hapa mjini Beijing, Kiswahili kilitumika rasmi kwa mara ya kwanza tangu ukumbi huo uzinduliwe mwaka 1959.

Katika ziara ya mama Samia nchini China mapema mwezi Novemba mwaka jana, pande hizi mbili zilitangaza kuinua uhusiano kati ya China na Tanzania hadi kuwa ushirikiano wa kimkakati wa kina.