Wizara ya Biashara na Maingiliano ya Kikanda ya nchini Ethiopia imesema, maonyesho ya biashara yatakayodumu kwa mwezi mmoja yatafanyika katika mji mkuu wa mkoa Tigray, Mekelle na miji ya Wukro, Adigrat na Maychew, ili kufufa shughuli za kibiashara katika kanda hiyo.
Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Ethiopia, maonyesho hayo, yatakayoanza Jumamosi wiki hii, yatafanyika chini ya kaulimbiu “Shughuli za Biashara za Tigray kwa ajili ya Amani ya Kikanda”.
Hatua hii inakuja baada ya usafiri kati ya mji mkuu wa Ethiopia, Addis Ababa na mji mkuu wa Tigray, Mekelle kuanza tena jumamosi iliyopita.